"JIRONGO ALIFARIKI KATIKA AJALI YA BARABARANI"-DCI

Idara Ya Upelelezi Wa Makosa Ya Jinai (Dci) Imedhibitisha Yakwamba Aliyekuwa Mbunge Wa Lugari Cyrus Jirongo Alifariki Kutokana Na Ajali Ya Barabarani Wala Sio Mauwaji Kama Inavyodaiwa.
Idara Ya Upelelezi Wa Makosa Ya Jinai (Dci) Imedhibitisha Yakwamba Aliyekuwa Mbunge Wa Lugari Cyrus Jirongo Alifariki Kutokana Na Ajali Ya Barabarani Wala Sio Mauwaji Kama Inavyodaiwa.
Katika Taarifa Iliyotolewa Na Idara Hio, Dci Imesema Uchunguzi Wa Kina Ulifanywa Ili Kubaini Hali Halisi Ya Kifo Hicho, Ikiwa Ni Pamoja Na Kuwahoji Wanandani Wake Jirongo Na Watu Waliokuwa Naye Kabla Ya Kifo Chake.
Timu Ya Uchunguzi Ilichukua Taarifa Kutoka Kwa Mashahidi Muhimu, Ikiwa Ni Pamoja Na Mkewe Ann Lanoi Pertet, Dereva Wa Basi Tiras Kamau Githinji, Kondakta Manoah Ekokwa Alukoya Olasi, Na Wafanyakazi Wa Kituo Cha Mafuta Cha Eagol, Ambapo Gari Lake Jirongo Lilionekana Likiwa Kabla Ya Ajali Kutokea.
Aidha, Spika Wa Bunge La Kitaifa Moses Wetang'Ula, Wanasiasa Rebman Malala Na Ibrahim Sambuli — Ambao Walionekana Naye Mara Ya Mwisho Kwenye Mkahawa Wa Karen Oasis Tarehe 12 Desemba 2025 Waliandikisha Taarifa Kwa Kilichotokea Usiku Huo.
Kando Na Hayo, Pia Idara Ya Dci Ilifanya Uchunguzi Wa Kina Katikakamera Za Cctv Na Pia Ushahidi Kutoka Katika Eneo La Ajali.
Kutokana Na Ushahidi Uliopatikana, Dci Imethibitisha Kuwa Tukio Hilo Lilikuwa Ajali Ya Kawaida Ya Barabarani, Bila Dalili Yoyote Ya Mauaji Au Mpango Wa Kumuua Jirongo.Idara Hiyo Ya Polisi Imesema Matokeo Ya Uchunguzi Huo Yatapelekwa Kwa Ofisi Ya Mkurugenzi Wa Mashitaka Ya Umma (Odpp) Ili Kupata Maelekezo Yanayofaa Baada Ya Kumalizika Kwa Hatua Zilizobaki Za Uchunguzi.
Jirongo, Ambaye Alikuwa Na Umri Wa Miaka 64, Alifariki Katika Ajali Mbaya Ya Barabarani Mapema Asubuhi Ya Desemba 13, 2025.Ripoti Zinaonyesha Kuwa Alikuwa Anaendesha Gari Lake Kuelekea Nyumbani Kwake Lugari Wakati Gari Lake Lilipogongana Ana Kwa Ana Na Basi La Climax Coach Kando Ya Barabara Kuu Ya Nairobi–Nakuru,Alizikwa Tarehe 30 Desemba Mwaka Uliopita Katika Eneo Bunge La Lugari Kule Lumakanda.


