WATU SITA WAFARIKI KATIKA AJALI YA BARABARANI KULE LONDIANI.

Watu Sita Wamefariki Dunia Na Wengine 46 Kujeruhiwa Hii Ni Baada Ya Basi Walilokuwa Wakisafiri Kugongana Na Lori.
Watu Sita Wamefariki Dunia Na Wengine 46 Kujeruhiwa Hii Ni Baada Ya Basi Walilokuwa Wakisafiri Kugongana Na Lori Katika Eneo La Tunnel Kwenye Barabara Ya Londiani Kuelekea Muhoroni Hii Leo Jumanne Asubuhi.
Akithibitisha Tukio Hili, Kamanda Wa Polisi Wa Kaunti Ya Kericho James Ngetich Amesema Ajali Ilitokea Baada Ya Basi La Uwezo Sacco Kugonga Nyuma Ya Lori Hilo Kwa Sababu Zisizojulikana Wazi.Ngetich Amesema Magari Yote Mawili Yalikuwa Yakielekea Upande Wa Kisumu.
Watu Sita — Abiria Watano Na Dereva Wa Basi — Wamefariki Dunia Papo Hapo, Huku Abiria 30 Wakipata Majeraha Mabaya Na Kusafirishwa Hospitalini Mbalimbali, Ikiwa Ni Pamoja Na Hospitali Za Londiani Na Fortenan.
Hata Hivyo Ngetich Amesema bado uchunguzi unaendelea kuhusiana na kilichosababisha ajali hio,huku akiwahimiza madereva kuwa waangalifu barabarani.


