Back to Home
County News

MARY EMASE AMKOSOA OKIYA OMTATAH

John MutanyiTuesday, 6 January 2026 at 15:1714 views
MARY EMASE AMKOSOA OKIYA OMTATAH

Mbunge Wa Teso Kusini, Mary Emaase, Amemkosoa Vikali Seneta Wa Kaunti Ya Busia , Okiya Omutatah.

Mbunge Wa Teso Kusini, Mary Emaase, Amemkosoa Vikali Seneta Wa Kaunti Ya Busia , Okiya Omutatah, Kwa Kuyumbisha Miradi Za Maendeleo Katika Eneo Bunge La Teso Kusini Na Busia Kiujumla.

Akizungumza Wakati Wa Kuzindua Zoezi La Kutoa Fomu Za Basari Kwa Wanafunzi Wa Shule Za Upili Eneo Bunge La Teso Kusini Emaase Amedai Seneta Omutatah Anapinga Kila Miradi Na Sera Za Serikali Ya William Ruto Hali Ambayo Ni Kizingiti Kwa Maendeleo Ya Wanabusia.

Hata Hivyo Amewataka Viongozi Kutoka Maeneo Ya Magharibi Kutopinga Ushirikiano Uliopo Baina Ya Rais William Ruto Na Viongozi Kutoka Mrengo Wa Upinzani (Broadbased) Ambapo Amehoji muungano huo ulikuwa Mapendeleo Ya Aliyekua Kiongozi Wa Chama Cha ODM Hayati Raila Odinga.