Back to Home
Politics

OKETCH AONDOA PENDEKEZO YA KUMTIMUA SIFUNA CHAMANI

John MutanyiTuesday, 6 January 2026 at 15:116 views
OKETCH  AONDOA PENDEKEZO YA KUMTIMUA SIFUNA CHAMANI

Seneta Wa Migori, Eddy Oketch, Ameaondoa Pendekezo Lake La Kumwondoa Seneta Wa Nairobi Edwin Sifuna Kama Katibu Mkuu Wa Chama Cha Odm

Seneta Wa Migori, Eddy Oketch, Ameaondoa Pendekezo Lake La Kumwondoa Seneta Wa Nairobi Edwin Sifuna Kama Katibu Mkuu Wa Chama Cha Odm, Na Kuamua Kusuluhisha Migogoro Inayoendelea Chamani Kupitia Vikao Vya Wanachama.

Kupitia Kwa Barua Iliyoandikwa Na Mwakili Wake, Oketch Ametangaza Kuwa Ameondoa Rasmi Ombi Hilo Ambalo Alikuwa Amewasilisha Hapo Jana.

Uamuzi Huu Umetokana Na Mashauriano Aliyofanya Na Kiongozi Wa Chama Cha Odm Na Seneta Wa Siaya, Dkt. Oburu Oginga.

Wakili Wake Oketch Wamesisitiza Kuwa Hatua Hii Inaheshimu Urithi Wa Kiongozi Mwanzilishi Wa Chama Hicho , Hayati Raila Odinga, Ambaye Alikuwa Akisisitiza Umuhimu Wa Mazungumzo Na Umoja Ndani Ya Chama.

Related Articles